1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Usiku wa tisa wa ghasia nchini Ufaransa

5 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELd

Ghasia mpya zimezuka nchini Ufaransa katika eneo lenye wakaazi wengi walio masikini,kaskazini mashariki ya mji mkuu Paris.Wafanya ghasia kwa siku tisa kwa mfululizo,wakati wa usiku wametia moto magari na majengo,licha ya askari polisi wengi kuwepo katika sehemu hizo.Ghasia sasa zimezuka pia katika maeneo mengine ya Ufaransa.Waziri Mkuu wa Ufaransa Dominique de Villepin akiwahotubia maafisa katika mkutano wa dharura amesema uhalifu wa aina hiyo nchini Ufaransa hautastahmiliwa.Hata waziri wa mambo ya ndani Nicolas Sarkozy amesema,hatua zitachukuliwa kuhakikisha kuwa sheria zinatekelezwa.Sasa askari polisi zaidi wanapiga doria mitaani katika maeneo yaliokumbwa na machafuko.Waliofanya ghasia hizo hasa ni vijana wa familia zilizohamia Ufaransa kutoka Afrika ya Kaskazini na wale wenye asili ya Kiafrika.Vijana hao wameghadhibika kwa sababu ya ukosefu mkubwa sana wa ajira na wanahisi kuwa wanabaguliwa kikabila.