1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Tufani yapiga kusini mwa Ufaransa.

7 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEdT

Sehemu za kusini mwa Ufaransa zimekumbwa na tufani kubwa iliyoambatana na mvua kubwa,zilizosababisha watu 1,500 kuhamishwa kutoka katika makazi yao.

Tufani hiyo imevuruga usafiri wa treni na ndege na maelfu ya watu hawana umeme.

Wataalam wa masuala ya hali ya hewa nchini Ufaransa,wamesema kiasi cha lita 400 za mvua kwa kila skwea mita imenyesha kwa kipindi kifupi sana.Mvua zaidi zimetabiriwa kunyesha katika siku chache zijazo.