1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Mkutano wa rais Chirac wa Ufaransa na Tony Blair wa Uingereza

7 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEU3

Waziri mkuu wa Uingereza amekutana na rais wa Ufaransa Jaque Chirac mjini Paris katika juhudi za kupunguza tofauti zao juu ya hatma ya Umoja wa Ulaya.

Katika mkutano wa pamoja na wanahabari waziri mkuu Blair ameuleza mkutano wake na Chirac kuwa uliokwenda vizuri na wenye manufaa.

Blair amekiri kwamba siku zote kunatokea kutoelewana ndani ya mataifa 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya lakini amesema anamatumaini kwamba mkutano usio rasmi wa viongozi wa mataifa wa Umoja huo atakaoungoza mjini London baadae mwezi huu huenda utakuwa na matokeo mazuri.