1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.Hotuba ya kwanza bungeni ya waziri mkuu wa Ufaransa Dominique

9 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF5O

Waziri mkuu wa Ufaransa Dominique De Villepin amesema atalipa kipaumbele suala la ukosefu wa ajira nchini humo.

Dominique ameyasema hayo katika hotuba yake ya kwanza kwenye bunge la Ufaransa.

Hotuba yake hiyo ilituwama sana katika suala hilo la Ukosefu wa ajira ingawa aligusia kuhusu kuendelea kujitolea kwa Ufaransa katika Umoja wa Ulaya,

Huku asilimia kumi ya watu wakiwa hawana ajira nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja alisema serikali imekuwa ikijikokota kuenda na wakati.

Dominique amechukua wadhifa huo baada ya nchi hiyo kuikataa katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.