1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTimor Mashariki

Papa Francis alakiwa kwa nderemo Timor Mashariki

9 Septemba 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amelakiwa kwa nderemo na vifijo nchini Timor Mashariki, ambapo anatarajiwa kuongoza misa kubwa.

https://p.dw.com/p/4kQAz
Timor ya Mashariki | Papa Francis akifurahia baada ya kufika mjini Dili
Papa Francis akionekana Timor Mashariki ni nchi ya tatu katika ziara yake ya siku 12 kwenye eneo la Asia na Pasifiki.Picha: Dita Alangkara/AP Photo/picture alliance

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ataongoza misa hiyo kubwa inayotarajiwa kuwaleta pamoja zaidi ya nusu ya watu milioni 1.3  wa nchi hiyo yenye Wakatoliki wengi.

Maalfu ya waumini walijipanga katika mitaa ya mji mkuu wa Timor Mashariki Dili, wakipeperusha bendera na miamvuli yenye rangi ya Vatican kumlaki Papa Francis, na msafara wake.

Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani, alionekana kuwamo katika hali ya uchangamfu alipotua, kutokea Papua New Guinea.

Timor Mashariki ni nchi ya tatu katika ziara yake ya siku 12 kwenye eneo la Asia na Pasifiki. Papa Francis anatarajiwa kuwahutubia viongozi wa Timor Mashariki na wanadiplomasia baadae leo, lakini kilele cha ziara yake kitakuwa misa kubwa ya pamoja hapo kesho Jumanne, ambapo waumini wapatao 700,000 wanatarajiwa kuhunduria misa hiyo.