1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Papa Francis atimiza miaka 10 ya uongozi

13 Machi 2023

Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis, Jumatatu hii anaadhimisha miaka kumi tangu alipochaguliwa kuliongoza kanisa hilo ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4Ob03
Vatikanstaat | Papst Franziskus, Generalaudienz
Picha: Andrew Medichini/AP Photo/picture alliance

Papa Francis, mwenye umri wa miaka 86, na raia wa Argentina, alikuwa papa wa kwanza kutoka Amerika ya kusini mnamo Machi 13 mwaka 2013, akimrithi Benedict XIV aliyestaafu na kufariki dunia mwishoni mwa mwaka jana.

Kardinali huyo wa zamani Jorge Mario ameamua kukuza maisha ya unyenyekevu katika uongozi wake. Hakuwahi kuchukua makazi ya kipapa yaliyotumiwa na watangulizi wake. Badala yake alisema anapendelea kuishi katika mazingira ya jamii kwa afya yake ya kisaikolojia.

Matatizo ya mara kwa mara ya goti yamemlazimisha kutumia mkongojo au kiti cha magurudumu, lakini hali yake ya afya inaonekana kuwa sawa.

Mnamo mwezi Mei mwaka uliopita, aliripotiwa kumwambia msaidizi wake kwamba huliongozi kanisa kwa kutumia goti, bali kwa kutumia kichwa.