1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVatican

Papa Francis asifu haiba ya upole ya mtangulizi wake

4 Januari 2023

Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis, amemsifia marehemu papa mstaafu Benedict wa Kumi na Sita kwamba alikuwa na mawazo safi na ya upole.

https://p.dw.com/p/4LjrC
Vatikan | Papst Franziskus
Papa Francis Picha: FILIPPO MONTEFORTE/AFP

Francis amesema hayo alipowaongoza maelfu ya waumini waliojitokeza kutoa heshima kwa marehemu Benedict, ambaye leo ni siku ya mwisho kwa mwili wake kutizamwa katika Kanisa la Mtakatifu Petero, Vatican.

Papa Francis alisema maelfu ya waliojitokeza, wanatoa heshima kwa aliyekuwa mwanatheolojia mahiri.

Tangu kifo chake siku ya Jumamosi, zaidi ya watu 130,000 wamejitokeza mjini Vatican kutoa heshima zao kwa papa huyo mstaafu, raia wa Ujerumani.

Hapo kesho, Papa Francis anatarajiwa kuongoza mazishi ya Benedict mjini Vatican, ambayo yatahudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali, licha ya ombi la Benedict alipokuwa hai kwamba akifa azikwe kwa hali ya kawaida.