1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis alazwa hospitali kwa changamoto ya upumuaji

Hawa Bihoga
30 Machi 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amelazwa hospitali siku ya Jumatano kutokana na maambukizi ya upumuaji ambayo itahitaji siku chache za matibabu.

https://p.dw.com/p/4PULN
Papst Franziskus
Picha: Stefano Spaziani/picture alliance

Msemaji wa Vatican Matteo Bruni amesema, katika siku za karibuni Papa Fracis amelalamika juu ya changamoto ya kupumua, lakini akisisitiza si Corona.Chanzo kutoka Vatican kimethibitisha kwamba  shughuli za Papa kwa siku ya Alhamis zilisitishwa,wakati huu ambao kumegubikwa shughuli nyingi kwa Papa kuelekea sikukuu ya Pasaka.

Licha ya uzee na changamoto za kiafya Papa Francis ameendelea kusafiri, ambapo mapema mwaka huu alifanya ziara nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Kongo na Sudan Kusini na kulakiwa na mamia kwa maelfu ya waumini,viongozi na wakuu wa nchi hizo.

Mwezi ujao, anatarajiwa kutembelea Hungary na kukutana na Waziri Mkuu Viktor Orban.