1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ahimiza amani Sudan

21 Mei 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo hii ametoa wito kwa makundi yanayopigana nchini Sudan kuweka kando silaha zao ili kufanikisha upatikanaji wa amani.

https://p.dw.com/p/4RdID
Pabst Franziskus PK Flugzeug Ungarn
Picha: Vatican Media via REUTERS

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo hii ametoa wito kwa makundi yanayopigana nchini Sudan kuweka kando silaha zao, akionyesha kusikitishwa na vurugu hizo ambazo zimeendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja katika taifa hilo la Afrika.Akizungumza na waumini katika uwanja wa kanisa la Mtakatifu Petro, Papa amepongeza makubaliano yaliyofikiwa hivi punde. Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha mazungumzo yanaendelea kufanyika ili kukomesha mateso kwa raia.Mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo hasimu Vikosi vya Msaada wa Dharura (RSF) yamesababisha kuvurugika kwa utawala wa sheria nchini humo.Lakini hata hivyo, Jana Jumamosi makundi hayo hasimu yalitia saini makubaliano ya kuweka chini mtutu wa bunduki kwa siku 7, hatua ambayo utekeleazji wake unatarajiwa kuanza kutekelezwa kesho Jumatatu.