1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shtayyeh: Misri haitamruhusu mtu yeyote kuingia kutoka Gaza

18 Februari 2024

Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Palestina, Mohammad Shtayyeh, ametoa wito kwa mamlaka ya Israel kuruhusu idadi ya watu waliojaa kusini mwa Ukanda wa Gaza kurejea makwao katika upande wa kaskazini.

https://p.dw.com/p/4cYE6
Ujerumani | Mkutano wa Usalama wa Munich | Mohammad Shtayyeh
Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Palestina Mohammad Shtayyeh akizungumza wakati wa Mkutano wa 60 wa Usalama wa Munich (MSC) huko Munich, kusini mwa Ujerumani Februari 18, 2024.Picha: THOMAS KIENZLE/AFP

Akizungumza katika Mkutano wa Usalama wa Munich, Shtayyeh alitoa onyo kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa asijaribu kulazimisha Wapalestina wavuke mpaka na kuingia Misri. Amesema anajua, na wanajua, kwamba imekuwa mpango wa Israeli kuwaondoa watu kutoka Gaza. Wao na Wamisri wamekuwa wakifanyajuhudi za pamoja kwa bidii ili jambo hilo lisifanikiwe. Kumekuwa na ripoti katika vyombo vya habari vya kimataifa kwamba Misri inajenga kambi ya mapokezi katika upande wake wa mpaka ili kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina.