1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Paetongtarn Shinawatra ndiye Waziri Mkuu mpya Thailand

16 Agosti 2024

Bunge la Thailand limemchagua Paetongtarn Shinawatra, binti wa bilionea na kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Thaksin Shinawatra, kuwa waziri mkuu.

https://p.dw.com/p/4jXTW
Thailand | Paetongtarn Shinawatra
Waziri Mkuu mpya Thailand Paetongtarn ShinawatraPicha: Sakchai Lalit/AP Photo/picture alliance

Akiwa na umri wa miaka 37, Shinawatra, atakuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchi humo na mwanamke wa pili kuwahi kushikilia wadhifa huo baada ya shangazi yake Yingluck.

Wabunge wamemuidhinisha Paetongtarn wa chama cha Pheu Thai kuwa waziri mkuu kwa kupata kura 319 dhidi ya 145 waliopinga. Kuchaguliwa kwake kunatokea siku mbili tu baada ya Waziri Mkuu wa zamani Srettha Thavisin kuondolewa na mahakama ya kikatiba.

Waziri Mkuu huyo mpya anakabiliwa na kibarua kigumu cha kufufua uchumi wa Thailand na kuepuka mapinduzi ya kijeshi na uingiliaji kati wa mahakama ambao umeondoa tawala nne zilizopita.