1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ongezeko la mfumuko lamaanisha njaa kwa watoto- uchunguzi

12 Oktoba 2023

Uchunguzi wa shirika ma msaada la World Vision umebainisha kwamba viwango vya juu vya mfumuko wa bei na kuongezeka kwa gharama za maisha kunachangia njaa duniani kote.

https://p.dw.com/p/4XRRU
World Vision: "Asilimia 59 ya wazazi waliohojiwa walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na njaa kwa watoto".
World Vision: "Asilimia 59 ya wazazi waliohojiwa walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na njaa kwa watoto".Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Ripoti ya uchunguzi huo uliofanyika kwenye mataifa 16 yaliyoidhinishwa umebaini kwamba asilimia 59 ya wazazi waliohojiwa walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na njaa kwa watoto pamoja na utapiamlo kwa familia zao huku asilimia 46 zikiwa hazijui pa kupata fedha za kununulia chakula.

Rais wa World Vision Andrew Morely amesema kwenye taarifa kwamba, hata kiwango cha watoto wanaolala bila ya kula kimepanda hadi asilimia 38 katika mataifa ya kipato cha chini, ingawa ameonya kwamba njaa ni tatizo la kiulimwengu.

Ulimwengu unatarajia kuadhimisha Siku ya Chakula, Jumatatu ijayo.