1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ongezeko la bei na uviko ndio sababu za umasikini Asia

24 Agosti 2023

Janga la UVIKO 19 na ongezeko la bei za vyakula na mafuta vimesababisha karibu watu milioni 70 katika mataifa yanayoendelea katika bara la Asia kukumbwa na umasikini uliopindukia mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4VXrz
Pakistan hohe Lebensmittelpreise an Ramadan
Picha: Mavra Bari/DW

Kwenye ripoti yake iliyoachapishwa Alhamis, Benki ya Maendeleo ya Asia imesema ingawa Asia na Pasifiki zinajikwamua kurejea katika hali ya kawaida baada ya janga la UVIKO-19, lakini kupanda kwa gharama za maisha kunadidimiza juhudi za kukabiliana na umasikini.

Mchumi mkuu wa benki hiyo ya ADB Albert Park amesema benki hiyo inakadiria watu milioni 155.2 miongoni mwa idadi jumla ya watu kwenye ukanda huo waliishi katika hali hiyo na huenda watu milioni 67.8 wasingeathirika kama majanga hayo yasingalitokea.

Benki hiyo yenye makao yake Manila, inauainisha umasikini wa kupindukia kuwa ni wa chini ya dola 2.15 kwa siku kulingana na mfumuko wa bei uliorekebishwa wa mwaka 2017.