1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Odinga azindua kampeni ya kuwania uongozi wa AU

27 Agosti 2024

Mchakato wa kuwania uongozi wa kamisheni ya Umoja wa Afrika umeanza rasmi baada ya Raila Odinga kuzinduliwa kuwa mwakilishi wa Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/4jyTh
Rais William Ruto akimpongeza Raila Odinga katika kampeni zake za kuwania uongozi wa AU
Rais William Ruto akimpongeza Raila Odinga katika kampeni zake za kuwania uongozi wa AUPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Mchakato wa kuwania uongozi wa kamisheni ya Umoja wa Afrika umeanza rasmi baada ya Raila Odinga kuzinduliwa kuwa mwakilishi wa Afrika Mashariki.

Odinga anashindana na wagombea wengine watatu wa kutoka Mauritius, Djibouti na Madagascar. Uchaguzi umepangwa kufanyika Februari mwakani. Marais 4 na wengine 2 waliostaafu wa Afrika wameidhinisha uteuzi wa Raila Odinga kuwania uongozi wa kamisheni ya Umoja wa Afrika.Mahakama Kenya yabatilisha muswada wa fedha wa 2023.

Soma: Kenya yaunda kamati ya ushindi ya Odinga

Hafla hiyo iliyofanyika kwenye ikulu ya Nairobi iliongozwa na Rais William Ruto iliwaleta pamoja marais 3 wa Afrika Mashariki akiwemo mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Salva Kiir, Yoweri Museveni wa Uganda na Samia Suluhu wa Tanzania.

Kwenye hotuba yake,mgombea wa uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Raila Odinga alisisitiza kuwa la msingi ni kulisogeza mbele bara kwa kujikita kwenye malengo ya pamoja badala ya tofauti zilizopo.

Raila Odinga wakati akizindua kampeni ya kuwania uongozi wa kamisheni ya AU
Kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga wakati akizindua kampeni ya kuwania uongozi wa kamisheni ya AUPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Odinga anafafanua kuwa ,”Niko tayari kuhudumu. Moyo wangu uko tayari na Niko imara. Kwa ushirikiano wenu nitaweza kuitumikia Afrika….asili ya binadamu. Afrika itaendelea ikiwa imeungana."

Odinga alibainisha kuwa azma yake ni kuwaunganisha waafrika na kuimarisha utekelezaji wa makubaliano yaliyopo. Kwa upande wake, rais wa Uganda Yoweri Museveni alisisitiza kuwa anaiunga mkono Kenya kuwania uanachama kwani vigezo vyote vimetimia.

Rais Museveni alihoji kuwa,"Tunakosa nini? Vyote vipo. Makabila yapo, madini yapo, masuala ya jinsia na wanawake yapo. Lazima kila mtu ajumuishwe kwenye harakati za kuzalisha mali na huduma.”

Odinga anachuana na waziri mkuu wa Djibouti Mahmoud Youssouf, Anil Gayan wa Mauritius na Richard Randriamandrato wa Madagascar. Kenya iliwasilisha rasmi ombi la kutaka kuwania uanachama wa AUC mwezi wa Julai mwaka huu.

Wakati huohuo, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alimpongeza Raila na kuweka bayana kuwa wako nyuma yake kwani, "Baba anatosha na achaguliwe.”

Odinga awasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Ruto

Mwenyeji wa hafla hiyo rais William Ruto alimsifu Raila Odinga kuwa na uzoefu, hekima na ujuzi wa kutosha aliye na imani na uwezo wa bara la Afrika na, "atafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuipa Afrika sifa na nguvu. Kadhalika ninazindua kikosi maalum cha uenezi kitakachoongozwa na Katibu wa wizara ya mambo ya kigeni Korir Singoei na balozi Elkanah Odembo."Umoja wa Afrika waonesha wasiwasi maandamano Kenya

Rais Ruto pia alibainisha kuwa sekretarieti maalum ikiongozwa na katibu katika wizara ya mambo ya kigeni Korir Singoei na balozi wa zamani wa Kenya nchini Marekani Elkanah Odembo ndiyo itakayosimamia kampeni.

Sekretariati hiyo itawajumuisha wanachama wanaotokea maeneo yote 5 ya Afrika. Nafasi ya mwenyekiti wa Umoja wa Afrika itakuwa wazi Februari mwaka 2025 baada ya Moussa Faki Mahamat wa Chad kuhitimisha muhula wake wa pili.