1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyalandu akihama chama cha CCM

30 Oktoba 2017

Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya chama tawala nchini Tanzania CCM na aliyekuwa Waziri wa Maliasili wa taifa hilo Lazaro Nyalandu amejiuzulu kutoka chama hicho.

https://p.dw.com/p/2mkzw

Nyalandu amejiuzulu kwa kile alichoeleza kuwa kutoridhishwa kwake na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini humo pamoja na ukiukwaji wa haki za binaadamu, ongezeko la vitendo vya dhulma wanavyofanyiwa baadhi ya Watanzania. Mwenzangu Sudi Mnette amezungumza na mwanasiasa Lazaro Nyalandu ambae anaelezea zaidi kuhusu uamuzi wake huo wa kujiuzulu ubunge na kujitoa  katika chama cha CCM. Sudi Mnette alizungumza na mbunge huyo.