1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni miaka 100 tangu vita ya kwanza ya dunia imalizike

Oumilkheir Hamidou
9 Novemba 2018

Vita vikuu vya kwanza vya dunia vimamalizika miaka 100 iliyopita.Tukio hilo ndio chanzo cha kumbukumbu  kubwa kabisa zitakazofanyika siku ya Jumapili nchini Ufaransa

https://p.dw.com/p/37y2E
Pariser Friedenskonferenz 1919 The Big Four
Picha: picture-alliance/AP Photo

Waingereza pia wanaandaa kumbukumbu zao. Na wajerumani wataikumbuka siku hiyo kwa kushirikiana na wenzao. Mnamo saa za mchana, Novemba 11 mwaka 1918 mwanajeshi wa kimarekani  Herny Nicholas Gunther alipigwa risasi  alipokuwa akiharakisha kufika katika kituo cha Ujerumani cha  kukusanya silaha huko Lothringe-ilikuwa saa tano kasoro dakika moja-dakika moja  tu kabla ya mkataba wa kuweka chini silaha kuanza kufanya kazi. Gunther anatajwa kuwa mhanga wa mwisho wa vita vikuu vya kwanza vya dunia, mmoja kati ya wanajeshi milioni kumi walioangukia mhanga wa vita hivyo. Lakini pia miongoni mwa raia wa kawaida, mamilioni wameuliwa.

Miaka mia moja baadae, mataifa yaliyoongoza vita wakati ule yanawakumbuka wahanga wa "Vita vikuu", kama vita vya kwanza vya dunia vinavyoitwa nchini Ufaransa na Uingereza. Wapi vinakumbukwa kwa aina gani vita hivyo, jibu linapatikana kupitia tathmini ya vita hivyo. Kwa Ufaransa na Uingereza vita vikuu vya kwanza vya dunia vinapewa umuhimu mkubwa zaidi kuliko nchini Ujerumani ambako  jukumu la kimaadili la balaa la yaliyotokea katika vita vikuu vya pili vya dunia na mauwaji ya halaiki dhidi ya wayahudi Holocaust linakamata mstari wa mbele. Katika kumbukumbu za miaka mia moja ya kumalizika vita vikuu vya dunia, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitumia fursa iliyojitokeza na kuigeuza nchi yake kuwa kitovu cha kumbukumbu za kimataifa.

Frankreich 100 Jahre Kriegsende Macron und Steinmeier in Straßburg
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier Picha: picture-alliance/dpa/L. Marin

Kuanzia leo Novemba kumi, rais Macron amepanga kukutana na kansela Angela Merkel katika mji wa kaskazini mwa Paris wa Compiègne kwa kumbukumbu fupi. Eneo hilo lina kumbukumbu mbili. Katika toto moja la treni ndiko makubaliano ya kuweka chini silaha yalipotiwa saini November 11 mwaka 1918 kati ya madola yaliyoshinda vita na utawala wa zamani wa ujerumani reich. Miaka 22 baadae, baada ya kuivamia Ufaransa, Adolf Hitler akawalazimisha viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo wasalim amri na mkataba kutiwa saini ndani ya toto hilo hilo la treni. Serikali ya Ufaransa lakini inataka kukumbuka tukio jengine la kihistoria:"Tunataka kufuata nyayo za Helmut Kohl na Francois Mitterand walipoingia  Verdun mwaka 1984."Kwa mujibu wa duru kutoka ikulu ya Ufaransa mjini Paris-Elysée. Tukio la kupeana mikono kansela wa wakati ule wa Ujerumani na rais wa wakati ule wa Ufaransa lilisifiwa ulimwenguni kama tukio la suluhu."

Paris 1919 Allierte Friedensverhandlungen
Viongozi wanne wakiwa wameketi mjini Paris mwaka 1919 wakijaribu kuanzisha mkataba wa amani wa Vita vya kwanza vya dunia.Picha: picture-alliance/AP

Kilele cha kumbukumbu za mwaka huu kitafikiwa kwa kufanyika kumbukumbui kubwa mjini Paris. Rais Macron amewaalika zaidi ya viongozi 80 wa taifa na serikali wa nchi tangu zinazohusika moja kwa moja  na vita vikuu vya kwanza vya dunia na pia zile ambazo hazihusiki moja kwa moja kushiriki katika kumbukumbu zitakazofanyika katika uwanja wa "Upinde wa Ushindi" au Arc de Triumph. Miongoni mwao wanatarajiwa rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.Viongozi hao wawili wanazozana kuhusu mkataba unaaopiga marufuku kumiliki makombora ya kinyuklia yenywe uwezo wa kushambulia hadi masafa ya kilomita 5500. Trump ametishia kujitoa katika mkataba huo. Viongozi wote wawili, na hivyo ndivyo rais Macron anavyotarajia, wataitumia fursa ya kumbu kumbu hizo ili kukutana na kuzungumza ili kuunusuru mkataba huo.

Ujerumani inawakilishwa katika hafla ambali mbali. Kansela Angela Merkel atashiriki katioka jukwaa la amani litakalofunguliwa na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres.. Kabla ya hapo rais wa shirikisho Frank-Walter Steinemeier alishiriki November nne iliyopita katika tamasha la muziki lililopewa jina tamasha la urafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani mjini Elsasse-eneo la Ufaransa lililokuwa likidhigitiwa na Ujerumanai katin ya mwaka 1871 hadi 1918.

Mwandishi: Hasselbach,Christoph/Hamidou Oummil

Mhariri: Mohammed Khelef