1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEWYORK: Koffie Annan aondolewa lawama.

30 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFS0

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffie Annan ameondolewa lawama katika kashfa ya mpango wa mafuta kwa chakula wa Iraq.

Ripoti iliyotolewa baada ya uchunguzi juu ya kashfa hiyo ilieleza kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hakuhusika na ushawishi wa kuipa tenda kampuni ya Cotecna kutoka Uswisi ambako mwana wa kiume wa Bwana Koffie Annan, Kojo Annan alikuwa akifanya kazi.

Lakini wakati huo huo ripoti hiyo imemlaumu bwana Koffie Annan kwa kutokulishughulikia swala hilo vilivyo.