1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York.Koffi Annan aamuru kusogezwa mbele uchaguzi nchini Ivory Coast kwa mara ya mwisho.

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1I

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ametoa mwito wa kurefushwa muda wa uchaguzi kwa mara ya mwisho nchini Ivory Coast na kusema ikiwa kura haikufanyika, Umoja wa Mataifa na viongozi wa Afrika watapendekeza serikali ya mpito isiyoegemea chama chochote.

Aidha katika taarifa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Annan amelitaka Baraza hilo kumuongezea mamlaka waziri Mkuu Charles Konan Banny.

Koffi Annan amelitolea mwito Baraza la Usalama kufikiria njia mpya za kuyashughulikia masuala mawili ya kutoa vyeti na kutayarisha orodha ya wapiga kura.

Taarifa hiyo yenye kurasa 26 imeelezea kwa ukamilifu juu ya taifa hilo la Afrika Magharibi, ambalo hapo awali lilikuwa ni la amani na neema na baadae kugawanyika kutokana na vita kulikopelekea kiasi cha watu laki saba kukosa makaazi na kutumbukia katika umasikini.