1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK:Iraq hatarini kutumbukia katika vita vikubwa aonya Kofi Annan

19 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDB3

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa bwana Kofi Annan kwa mara nyingine tena ameonya kwamba Iraq iko katika hatari ya kutumbukia katika vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.

Annan ametoa onyo hilo baada ya watu zaidi ya arobaini kuuwawa hapo jana jumatatu katika mashambulio tofauti ya mabomu.

Watu 22 waliuwawa kaskazini mwa mji wa Tal-Afar wakati mtu mmoja alipojitoa muhanga kwa kujiripua katikati ya soko lililokuwa limejaa watu.

Mjini Ramadi magharibi mwa mji wa Baghdad,watu 13 waliuwawa baada ya bomu kuripuliwa nje ya kituo cha polisi.Mapema jumatatu pia watu wengine wanane waliuwawa kufuatia mashambulizi ya mabomu na risasi katika mji wa Baquba ulioko kaskazini mashariki mwa mji wa Baghdad.