NEW YORK:Bhuto ataka kurejea Pakistan
1 Aprili 2007Matangazo
Aliyekuwa waziri Mkuu wa Pakistan bibi Benazir Bhuto amesema anakusudia kurejea nchini humo mwaka huu licha ya uwezekano kwamba anaweza kutiwa ndani.
Bibi Bhuto amesema itakuwa heshima kwake ikiwa atachaguliwa tena kuwa waziri mkuu.Waziri Mkuu huyo wa zamani amewaambia waandishi habari mjini New York kuwa hafikiri kuwa anaweza kukamatwa.