1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mrithi wa Annan ajulikane ifikapo Oktoba

28 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD8A

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubali kuwa mrithi wa Katibu Mkuu Kofi Annan,lazima achaguliwe hadi mwisho wa mwezi Oktoba.Kati ya wagombea 7,alieshika nafasi ya mbele katika chaguzi mbili zisizo rasmi katika Baraza hilo lenye wanachama 15,ni waziri wa mambo ya kigeni wa Korea ya Kusini,Ban Ki-Moon.Yeye ameapa kupunguza urasimu na kufanya mabadiliko yatakayosaidia kazi kufanywa kwa mafanikio zaidi. Mwezi wa Desemba,Kofi Annan anakamilisha miaka yake kumi kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.