1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK. Miripuko ya New York huenda iwe na uhusiano na mzozo wa Israel na Palestina.

6 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFG8

Polisi mjini New York, Marekani wamesema miripuko iliyotokea nje ya ubalozi mdogo wa Uingereza ilisababishwa na makombora ya kutengenezwa nyumbani.

Mkuu wa polisi mjini humo, Raymond Kelly, amewaambia waandishi habari kwamba anafanya uchunguzi katika kampuni linaloiuzia matinga tinga Israel, ambayo yanatumiwa kuyabomoa makazi ya wapalestina. Amesema kundi la wayahudi wanaopinga hatua ya Israel kuyakalia maeneo ya Palestina lilifanya maandamano nje ya jengo hilo mnamo tarehe 13 mwezi uliopita.

Tukio hilo limeutilia shaka usalama wa mji wa New York, licha ya usalama kuimarishwa tangu shambulio la tarehe 11 mwezi Septemba mwaka wa 2001. Polisi wanaufanyia uchunguzi ukanda wa video unaomuonyesha mwendesha baiskeli akiwasha moto na kuyatupa makombora hayo kuelekea kwenye jengo hilo, kabla kukimbia.