1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Kura rasmi kumchagua mrithi wa Annan

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5o

Waziri wa nje wa Korea ya Kusini Ban Ki-Moon,ni mgombea pekee aliebakia kuwa mrithi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan.Baada ya Ban Ki-Moon kufanikiwa katika kura ya majaribio kwenye Baraza la Usalama,wagombea wengine wamejitoa katika kinyanganyiro hicho.Siku ya Jumatatu,kura rasmi itapigwa kumchagua mrithi wa Annan.