1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Koffi Annan ahofia vita kuzuka tena Cote d' Ivoire-

25 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFyD

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Umoja wa mataifa, Bwana Koffi Annan, amesema kuna hatari kubwa ya vita kuzuka tena nchini Cote d' Ivoire, ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa. Katika mkutano na wajumbe katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa mjini New York, Bwana Koffi Annan, amesema ikiwa hatua hazitachukuliwa ili kupata suluhu la mizozano iliyopo wakati huu, baina ya pande zinazohasimiana nchini Cote d'Ivoire, basi vita vitalipuka tena.

Wawakilishi wa vyama vya waasi wanaopinga utawala wa Rais laurent Gbagbo, ambao mwezi Aprili uliopita walikua wamekubali kushiriki katika baraza la mawaziri wa serikali ya mpito, tangu mwezi september wanasusia serikali hio, kwa madai kwamba Rais Gbagbo amekua akiendesha njama za kuvuruga makubaliano yaliyofikiwa Marcoussis-Ufaransa-

Wajumbe wa Jumuia ya CEDEAO au ECOWAS, ya uchumi wa mataifa ya magharibi mwa bara la Afrika, Jumuia ambayo imekua ikijaribu kupatanisha serikali ya Abidjan na wapinzani wake, wamependekeza kipelekwe nchini Cote d'Ivoire kikosi cha jeshi la kimataifa; lakini Bwana Annan amesema atalijadili pendekezo hilo, kabla ya kulikabidhi baraza la usalama.