1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Bill Clinton ateuliwa kuwa mjumbe maalum wa tsunami.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNX

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffie Annan amemtaja rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton kuwa mjumbe maalum wa umoja wa mataifa atakaeshugulikia maswala ya janga la tsunami.

Bill Clinton akizungumza katika makao makuu ya umoja wa mataifa mjini New York alisema kuwa shida nyingi zilizolikumba bara la Asia baada ya Tsunami bado hazijatatuliwa na akaitaka jamii ya kimataifa isipoteze muelekeo.

Katibu mkuu Koffie Annan alisema kuwa kazi kubwa itakayo mkabili Clinton ni kuwasiliana na mataifa yaliyoathirika na mataifa wafadhili ili kuona kuwa misaada inaendelea kutolewa kwa ajili ya ujenzi mpya wa mataifa yaliyoathirika.