1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Annan awataka viongozi wa serikali kusaidia kuipa sura ya kisasa taasisi hiyo ya kimataifa.

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6x

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Kofi Annan ametoa tena wito kwa viongozi wa serikali kusaidia kuipa sura ya kisasa taasisi hiyo ya umoja wa mataifa.

Amesema kuwa taasisi hiyo inapaswa kuchukua hatua madhubuti kupunguza umasikini duniani kwa kiwango cha nusu hadi kufikia mwaka 2025 na kupambana na ugaidi wa kimataifa.

Pia amesema kuwa ana imani kuwa umoja wa mataifa utaidhinisha ajenda yake muhimu ya mageuzi katika mkutano wake wa Septemba mjini New York.