1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York: Annan akutana na kikundi cha ushauri:

2 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFw5

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, kwa mara ya kwanza amekutana na Mabalozi wa kikundi cha ushauri kilichoteuliwa kushughulikia mgogoro wa Irak. Anataka kupima kama wakati wa muwafaka umewaidia wa kuitisha mkutano wa kimataifa kuhusu mustakabali wa Irak. Kikundi cha ushauri kina nchi 17 na nyingi kati yao ni zile ambazo ni jirani na Irak. Wajumbe wengine wa kikundi hicho ni wanachama wote wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na wale wanaobadilishwa kila baada ya miaka miwili. Ujerumani ni miongoni mwa Wajumbe wa kikundi hicho.