1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Annan afungua mkutano kuhusu wahamiaji.

15 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCJ

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amefungua mkutano wa kwanza wa dunia wa uhamiaji. Akihutubia wajumbe wa mkutano huo wa siku mbili mjini New York, Annan , amezitaka serikali duniani kote kulishughulikia suala la wahamiaji kupitia mazungumzo na ushirikiano badala ya upinzani.

Katika ripoti yake ya hivi karibuni , umoja wa mataifa unakadiria kuwa kiasi cha watu milioni 200 wako nje ya nchi zao za uzawa. Idadi kubwa ya wakimbizi inaishi katika mataifa ya Ulaya ikifuatiwa na Marekani na Asia.

Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na wasi wasi kuwa Waafrika zaidi wanaotarajiwa kuwa wahamiaji wanakimbilia Ulaya, huku mara nyingi wakihatarisha maisha yao katika hatua hiyo.