1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Annan afadhaishwa na vita Sri Lanka

15 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDLP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema amefadhaishwa na kuendelea kupamba moto kwa umwagaji damu nchini Sri Lanka.

Katika shambulio la hivi karibuni kabisa watu saba wameuwawa na wengine 17 kujeruhiwa baada ya bomu kuripuka katika mji mkuu wa Colombo.Serikali ya Sri Lanka imesema waasi wa Tamil Tigers wanahusika na shambulio hilo ambalo linadaiwa kuulenga msafara wa balozi wa Pakistan nchini humo.Mripuko huo umetokea muda mfupi baada ya waasi wa Tamil Tigers kuishutumu serikali kwa kupiga mabomu nyumba ya mayatima katika eneo linalodhibitiwa na waasi na kuuwa watoto 61.Serikali imekanusha madai hayo kwa kusema kwamba kikosi chake cha anga kilikuwa tu kimeshambulia kituo cha mafunzo cha waasi.

Mamia ya watu wameuwawa katika wimbi la hivi karibuni la umwagaji damu nchini humo.