1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI:Waziri wa nje wa India aondoka madarakani

8 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKc

Waziri wa mambo ya kigeni wa India,Natwar Singh amelazimishwa kuondoka madarakani baada ya jina lake kutajwa katika ripoti huru inayohusika na ukiukaji wa mpango wa Umoja wa Mataifa uliyoiruhusu Iraq kuuza mafuta ili iweze kununua chakula.Waziri mkuu wa India Manmohan Singh atashika wadhifa wa Natwar Singh kabla ya kufanywa mkutano muhimu wa kilele wa kanda hiyo mwishoni mwa wiki hii nchini Bangladesh.Natwar Singh atabakia katika baraza la mawaziri bila ya wadhifa,mpaka matokeo ya uchunguzi unaofanywa yatakapopatikana.Kwa upande mwingine maafisa wa Kijerumani wameanza kumchunguza mfanya kazi wa zamani wa shirika la DaimlerChrysler kuhusika na gari iliyouziwa Iraq,wakati ambapo nchi hiyo iliwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.Mwajiriwa huyo wa zamani wa DaimlerChrysler,anashukiwa kwamba kinyume na sheria,alipata kibali cha kuisafirisha nje gari hiyo kwa msaada wa malipo ya siri.