1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New delhi.Mfululizo wa miripuko wauwa watu kadhaa nchini India.

8 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEE

Kiasi cha watu 35 wamefariki katika mfululizo wa miripuko iliotokea nchini India magharibi mwa jimbo la Maharashtra.

Polisi wamesema kuwa wametoa amri ya kutotoka nn’je na wanausalama wametumwa katika mji wa Malageon baada ya miripuko miwili hadi mitatu katika mji wa Malegaon, moja kati ya miripuko hiyo umeripotiwa kutokea nn’je ya msikiti.

Miripuko hii imetokezea siku chache tu baada ya waziri mkuu wa India Manmohan Singh kusema kwamba shirika la upelelezi limetahadharisha kuwepo kwa uwezekano wa kufanywa mashambulizi ya kigaidi kateka maeneo kadhaa nchini humo.

Mnamo mwezi wa July zaidi ya watu 180 walifariki kutokana na mfululizo wa mabomu yaliyotegwa kwenye treni katika mji mkuu wa jimbo la Maharashtra, Mumbai.

Wakati huo huo maafisa nchini India wamesema, zaidi ya wachimbaji migodi 50 wamefariki baada ya kutokea mripuko katika machimbo ya makaa ya mawe huko mashariki mwa mji wa Jharkand.

Imeelezewa mrundikano wa gesi ya methane na carbon dioxide ndio uliopelekea mripuko huo, huku waokoaji wakielezea khofu yao ya kuwapata wachimbaji waliosalimika.