1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndoto ya robo fainali ya Dortmund yazimwa na Chelsea

8 Machi 2023

Safari ya klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, Borussia Dortmund katika ligi ya mabingwa barani Ulaya imefika mwisho katika hatua ya 16 bora baada ya kuondolewa katika mashindano hayo na Chelsea.

https://p.dw.com/p/4ONj2
FC Chelsea - Borussia Dortmund
Picha: David Inderlied/dpa/picture alliance

Safari ya klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, Borussia Dortmund katika ligi ya mabingwa barani Ulaya imefika mwisho katika hatua ya 16 bora baada ya kuondolewa katika mashindano hayo na Chelsea.

Katika mechi iliyochezwa uwanjani Stamford Bridge huko mjini London, Chelsea waliingia uongozini kupitia kwa Raheem Sterling halafu Kai Havertz akaongeza goli la pili kupitia mkwaju wa penalti uliokuwa na utata ambao alilazimika kuupiga mara mbili.

Dortmund waliwasili katika mechi hiyo wakiwa kifua mbele kwa goli moja baada ya kupata ushindi katika mechi ya raundi ya kwanza. Miamba hao wa Ujerumani walikuwa katika msururu wa mechi kumi bila kushindwa mashindano yote wanayoshiriki.