1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amani ya Afghan mashakani kufuatia kuongezeka kwa mapigano

21 Oktoba 2020

Jumuiya ya Kujihami ya NATO imesema vikosi vyake havitaondoka Afghanistan, mpaka hali ya kiusalama itakaporuhusu, pamoja na kwamba vikosi vya  Marekani vinatarajiwa kuondoka huko katika kipindi cha Sikukuu ya Krismasi.

https://p.dw.com/p/3kFSY
Brüssel Jens Stoltenberg NATO-Generalsekretär
Picha: Dursun Aydemir/AA/picture alliance

Katibu Mkuu wa Umja huo, Jens Stoltenberg  amesema katika kuhakikisha mipango kuhusu nusura ya taifa hilo inaakwenda vyema wataazingatia kanuni yaa kufanya kazi kwa pamoja na endaapo mazingira yatawaaruhusu wataondoka paamoja nchini Afghanistan.

Trump asema Marekani itabakisha kikosi madhubuti.

Mapema Oktoba 7, kupita ukurasa wake wa Twetter, Rais Donald Trump wa Marekani, alinadikia hadi kufikia katika kipindi cha Krismas tafaa lake litakuwa limiwabaabisha wanajeshi waachaache madhubuti.

NATO imekuwa ikiongoza jitihada ya ulinzi wa amani ya kimataifa nchini Afghanistan tangu 2003, ikiwa ni takriban miaka miwili baaada ya muungano wa kijeshi uliokuwa ukiongozwa na Marekani kuwaondoa wapiganaji wa Taliban. Wapiganaji haao ndio walikuwa wakimpaa hifadhi aliyekuwa kiongozi waa kundi la al-Qaeda Osama bin Laden. 

Hadi kipindi hiki vikosi 12,000 kutoka mataifa 38 tofauti duniani vipo nchini Afghanistan. Pamoja na mambo mengine wanajeshi hao wanafanya kazi ya kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama wa taifa wa taifa hilo. Kwa sehemu kubwa Marekani inaafanya takribani nusu ya wanajeshi ambao wanashiriki operesheni.

Je, NATO inaaweza kufanya kazi Afghanistan bila ya Marekani?

Afghanistan US-Truppen
Baadhi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan Picha: picture-alliance/Getty Images/T. Watkins

Kuna vikosi 8,000 vya Marekani ambavyo vimehusika katika operesheni za hivi karibuni  za NATO pamoja na washirika wake. Duru zinaeleza kwa kiasi kikikubwa vikosi hivyo vinaitegemea Marekani katika masuala mbaalimbali kuanzia nguvu za anga, usafiri na msaada wa kimatibabu, jambo ambalo linaoneshaa ishara ya kwamba upo uwezekano wa operesheni hiyo kutoafnikiwa vyema pasipo uwepo wa  Marekani.

Wanadiplomasia na maafisa kijeshi wamekuwa na wasiwasi kwamba kuondoka kwa Marekani katika ardhi ya Afghanistan kunaweza kutatiza jitihaada za kutafuta amani kati ya serikali ya Afghanistan na Taliba. Mkanganyiko kuhusu kuondoka kwa vikosi katika kile kinachojulikana vitaa ya muda mrefu zaidi ya Marekani unaahusisha pia suala la nyeti la kifamilia miongoni wa wanajeshi wa Marekani.

Juma lililopia mshauri wa masuala ya usalama wa Trump alisikika akisema vikosi vitapunguzwa haadi kufikia 2,200 itakapofikia mapema mwaka ujao. Lakini wanadiplomaasia wa NATO wanaonesha uwezekano wa vikosi hivyo kubakia nchini Afghanistan hadi katikati ya mwaka ujao wa 2021.

Mwandishi: Sudi Mnette/ AP