1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NANCY,UFARANSA: Katiba ya Umoja wa Ulaya

20 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFC8

Kansela wa Ujerumani bwana Gehard Schröder ametoa mwito kwa wananchi wa ufaransa waikubali katiba mpya ya Umoja wa Ulaya watakapopiga kura ya maoni mnamo siku kumi zijazo.

Kansela wa Ujerumani alitoa mwito huo jana kwenye mkutano na marais wa Ufaransa na Poland uliofanyika katika mji wa Nancy nchini Ufaransa.

Hatahivyo kura za maoni hadi sasa zinaonyesha kwamba wananchi wa Ufaransa bado wamegawanyika juu ya suala la katiba ya Umoja wa Ulaya.

Ili katiba hiyo iweze kutumika,nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya zinapaswa kuikubali.

.