1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Mazungumzo kati ya ujumbe wa serikali ya Uganda na LRA kuanza leo

8 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDNo

Msemaji wa ujumbe wa serikali ya Uganda, kapteni Paddy Ankunda, amesema mazungumzo kati ya ujumbe huo na wajumbe wa kundi la waasi la LRA, yanatarajiwa kuanza leo mjini Juba kusini mwa Sudan.

Mazungumzo hayo yalicheleweshwa jana wakati wajumbe wa serikali ya Uganda waliposhauriana na maofisa wa serikali ya Sudan. Serikali ya Uganda pamoja na mpatanishi mkuu katika mazungumzo hayo, makamu wa rais wa Sudan, Riek Machar, ilimtaka kiongozi wa LRA, Joseph Kony au makamu wake, Vincent Otti, washiriki katika mazungumzo hayo.

Hata hivyo, viongozi hao wanaotafutwa kwa uhalifu wa kivita na mahakama ya kimataifa ya jinai mjini Hague, wamejificha katika misitu nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.