1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Naibu mwenyekiti wa chama cha EFF ajiunga na chama cha Zuma

15 Agosti 2024

Makamu kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters EFF nchini Afrika Kusini, Floyd Shivambu, ametangaza kuwa anajiuzulu kutoka kwenye chama hicho.

https://p.dw.com/p/4jWPU
Msukosuko waingia ndani ya chama cha EFF cha Julius Malema
Msukosuko waingia ndani ya chama cha EFF cha Julius MalemaPicha: Alet Pretorius/REUTERS

Kuondoka kwa Shivambu katika chama hicho kinachoongozwa na Julius Malema ni pigo kubwa. Kuondoka huku kwa Shivambu kunaashiria mvuto unaoongezeka katika chama cha MK ambacho kwa sehemu kubwa kina umaarufu katika mkoa wa KwaZulu Natal anakotokea Zuma.

Chama cha EFF kupitia kiongozi wake Malema kimesema chama hicho kinapitia majaribu na lazima kiyashinde, la sivyo kitaangamia.