1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nagelsmann asema hataruhusu mjadala juu ya makosa ya Neuer

8 Juni 2024

Kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann amesema hataruhusu mjadala wowote kuhusu kosa jingine lililofanywa na mlinda lango namba moja Manuel Neuer, katika mechi ya kirafiki na Ugiriki, kabla ya michuano ya Euro 2024.

https://p.dw.com/p/4goBt
Mechi za kirafiki kabla ya Euro 2024
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Julian Nagelsmann afunga mjadaa juu ya makosa yanayodaiwa kufanywa na mlinda lango namba moja Mauel NeuerPicha: Titgemeyer/osnapix/IMAGO

Neuer, alishindwa kulizuia kombora la Christos Tzolis katika dakika ya 33 baada ya safu ya ulinzi ya Ujerumani kupoteza mpira karibu na eneo la hatari na kuwapa fursa ya kuandika bao la kwanza.

Hata hivyo Ujerumani walimaliza mechi hiyo na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Kai Harvetz na Pascal Gross, aliyefunga katika dakika za majeruhi.

Neuer analaumiwa pia kwa kufanya makosa siku ya Jumatatu walipokutana na Ukraine, na hata kwenye michuano ya Champions, wakati Bayern Munich ilipokutana na Real Madrid katika nusu fainali hivyo kuwapa nafasi Madrid kusonga mbele.

Hata hivyo Nagelsmaann amekwishasema Neuer atakuwa namba moja kwenye michuano ya Euro inayoanza Ijumaa ijayo, watakapokutana na Scotland.