Machafuko ya kisiasa nchini Msumbiji yameongezeka huku taifa hilo likikaribia siku ya kuapishwa kwa Rais Mteule Daniel Chapo tarehe 15 Januari. Taifa hilo la kusini mwa Afrika sasa linakabiliana na mgogoro wa wakimbizi, kutoroka kwa wafungwa wengi gerezani, na ghasia za kila mahali ambazo zimegharimu maisha ya watu zaidi ya 250 tangu uchaguzi wa Oktoba uliogubikwa na utata.