1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwili wa Papa Benedict waagwa Vatican

2 Januari 2023

Waumini wa Kanisa Katoliki leo watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho mjini Vatican kwa Papa Benedict wa 16.

https://p.dw.com/p/4Ld95
Vatikan Aufbahrung Papst Benedikt
Picha: Vatican Media/ANSA/ZUMA Press/picture alliance

Mwili wa Papa Benedict utalazwa kwa siku tatu katika kanisa kuu la Mtakatifu Petro kabla ya mazishi yake.

Kiongozi huyo wa kidini ambaye ni raia wa Ujerumani, aliyefariki siku ya Jumamosi akiwa na umri wa miaka 95, aliliongoza kanisa Katoliki kwa muda wa miaka minanne kabla ya kuwa Papa wa kwanza katika kipindi cha karne sita kujiuzulu mnamo mwaka 2013.

Mrithi wake Papa Francis ataongoza ibada ya mazishi siku ya Alhamisi katika uwanja mkuu wa Mtakatifu Peter, kabla ya kuzikwa kwenye makaburi yaliyoko katika kanisa la mtakatifu Petro.

Papa Benedict alifariki katika nyumba ya watawa ya Mater Ecclesiae ndani ya bustani ya Vatican, ambayo yalikuwa makaazi yake kwa muongo mmoja uliopita.