1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwenyekiti wa kamisheni kuu ya Umoja wa Ulaya Barroso awasihi wafaransa waunge mkono katiba ya Ulaya

18 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFCK

Mwenyekiti wa kamisheni kuu ya Umoja wa ulaya,José Manuel Barroso amewatolea mwito wafaransa waunge mkono katiba ya umoja wa Ulaya kura ya maoni itakapoitishwa may 29 ijayo.“Kura ya ndio ni ushahidi wa imani ya Ufaransa kwa ulaya na ishara ya hali biora ya siku za mbele kwa Ufaransa“ amesema bwana Barroso katika mahojiano na kiuto kimoja cha matangazo ya radio cha ufaransa.Mwenyekiti wa kamisheni kuu ya Umoja wa Ulaya ameondowa uwezekano wa kujadiliwa upya mkataba wa ulaya pindi wafaransa wakiipinga katiba.Yadhihirika kana kwamba utaratibu wa kuipigia kura katiba hiyo utaendelea hata kama wafaransa wataipinga.Wakati huo huio mtangulizi wa bwana Barroso,Romano Prodi amezungumzia hofu ya kuzuka kizungumkuti cha kisiasa ikiwa wafaransa wataipinga katiba ya umoja wa ulaya.