1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha maarufu wa Uganda Benjamin Kiplagat afia Kenya

31 Desemba 2023

Mwanariadha maarufu wa Uganda Benjamin Kiplagat ameaga dunia nchini Kenya, na vyombo vya habari nchini humo vinaarifu kuwa ameuawa.

https://p.dw.com/p/4akPw
Deutschland | Protestaktion Letzte Generation | beim Berlin-Marathon 2023
Picha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Polisi ya Kenya imesema mwili wa mwanariadha huyo umekutwa ndani ya gari usiku wa kuamkia leo, nje kidogo ya mji wa Eldoret katika ukanda wa Bonde la Ufa.

Kamanda wa polisi katika eneo hilo, Stephen Okal ameviambia vyombo vya habari kuwa maafisa wengi wamepelekwa katika eneo la tukio, wakiendesha uchunguzi kujua mazingira ya kifo cha Kiplagat.

Okal amesema mwili wa Kiplagat ulikuwa na jeraha kubwa shingoni, ikiwa ishara kuwa alichomwa kisu. Benjamin Kiplagat ambaye ni mzaliwa wa Kenya, aliiwakilisha Uganda katika mashindano ya kimataifa, zikiwemo mbio za nyikani za mita 3000.

Alikuwa na umri wa miaka 34.