1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUfaransa

Mwanadiplomasia wa Ufaransa ataka kusitishwa mapigano Gaza

17 Desemba 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Catherine Colonna ametoa mwito wa kupatikana makubaliano ya "haraka na yatakayodumu kwa muda mrefu" ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4aGkC
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Catherine Colonna
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Catherine ColonnaPicha: Vahram Baghdasaryan/Photolure via REUTERS

Colonna ametoa matamshi hayo mjini Tel Aviv baada ya mazungumzo na waziri mwenzake wa Israel Eli Cohen na kuongeza kuwa raia wengi wanauliwa kwenye ardhi hiyo ya Wapalestina.

Mwanadiplomasia huyo wa Ufaransa atakayelitembelea pia eneo la Ukingo wa Magharibi amezihimiza pande zote kusitisha makabiliano akisema hakuna atakayenufaika iwapo hali ya mzozo huo itazidi kuwa mbaya na kusambaa kwenye kanda nzima

Colonna pia amesisitiza kwamba waathirika wa mashambulizi ya Hamas ya Okotba 7 ndani ya ardhi ya Israel hawapaswi kusahaulika ikiwemo wale inaotajwa kuwa walifanyiwa ukatili wa kingono na wapiganaji wa Hamas.