1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanadiplomasia mkuu wa Saudia awasili Tehran

17 Juni 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia amewasili mjini Tehran, Iran hii leo, ikiwa ni hatua ya karibuni katika mchakato wa kurejesha mahusiano ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili hasimu ya Mashariki ya Kati

https://p.dw.com/p/4SihA
Iran Teheran | Außenminister: Hossein Amirabdollahian und Prince Faisal
Picha: Vahid Salemi/AP/picture alliance

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kwamba mwanadiplomasia huyo wa juu wa Saudi Arabia mwanamflame Faisal bin Farhan alikaribishwa rasmi na mwenzake wa Iran, Hossein Amirabdollahian.

Kiongozi huyo anatarajia kukutana na rais Ebrahim Raisi kumpatia ujumbe kutoka kwa mfalme wa Saudi Arabia baadae leo, hii ikiwa ni kulingana na kituo cha televisheni cha Iran.

Ziara hiyo inafanyika baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken kuzuru Saudi Arabia mapema mwezi huu. Mwezi Machi, Iran na Saudia zilikubaliana kurejesha upya mahusianio ya kidiplomasia na kufungua tena balozi zao baada ya miaka saba ya mivutano.