1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanachama wa ETA atiwa nguvu Ufaransa

3 Aprili 2004
https://p.dw.com/p/CFe1
PARIS: Huko Ufaransa ya Kusini polisi wamemtia nguvuni mojawapo wa washutumiwa wa kigaidi wanaotafutwa sana wa chama cha chini kwa chini cha Kibaski ETA, kinachopigana vita vya kujitenga. Polisi walisema aliyetiwa nguvuni ni mkuu wa kuwiyanisha mawasiliano ya makomando wa ETA, Felix Alberto Lopez de Lacalle. Lopez de Lacalle mwenye miaka 43 anayeitwa kwa jina lake la kificho Mobutu anashutumiwa kupangilia njama kadha za mashambulio. Mwishoni mwa mwaka 2000 Lopez de Lacalle alikuwa akabidhiwa Uspania baada ya kutiwa ndani miaka saba nchini Ufaransa, lakini aliweza kutoroka jela.