Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen, umekataa pendekezo la kusitisha mapigano na waasi wa Kihouthi, ukisema waasi hao wa Kishia wanaoungwa mkono na Iran hawana nia ya dhati na wanaendeleza operesheni za kivita licha ya kudai wanataka amani.