1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Mtuhumiwa akiri kupanga mauaji ya rais wa Haiti

25 Machi 2023

Mtuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya amekiri kushiriki mauaji ya aliyekuwa rais wa Haiti Jovenel Moise.

https://p.dw.com/p/4PEUj
Haiti Ermordung Präsident Moise Witwe First Lady Martine Moise
Picha: Joseph Odelyn/AP Photo/picture alliance

Rodolphe Jaar amekiri mauaji hayo katika mahakama ya Miami nchini Marekani kwa kutoa vifaa na kula njama ya kumteka na kumuua rais Moise, hii ikiwa ni kulingana na rekodi za mahakama.

Mtuhumiwa huyo raia wa Chile na Haiti ni wa kwanza kati ya 11 wanaotuhumiwa kwa kuandaa mauaji hayo na hukumu yake huenda ikatolewa Juni 2.

Raia wengi tayari wamekamatwa nchini Haiti, lakini kesi zao zimesimama baada ya majai kutishiwa kuuawa. Jovenel Moise alipigwa risasi mara 12 akiwa nyumbani kwake karibu na makao makuu ya Haiti, Port-au-Prince, Julai 7, 2021.