1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akutwa ameuawa Tanzania

18 Juni 2024

Hofu yatanda Tanzania miongoni mwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi kufuatia tukio la mtoto wa umri wa miaka miwili ambaye mwili wake ulipatikana Jumatatu katika wilaya ya Muleba, ukiwa hauna baadhi ya sehemu za viungo vyake. Mtoto huyo anadaiwa kutekwa mikononi mwa mamake mnamo Mei 30. Jacob Safari amezungumza na mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania Godson Molel kuhusu tukio hilo.

https://p.dw.com/p/4hCOc