1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani aitembelea China

27 Agosti 2024

Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani,Jake Sullivan ameitembelea China, ni ziara yake ya kwanza nchini humo katika kipindi cha miaka minane.

https://p.dw.com/p/4jxNV
China Peking | Jake Sullivan
Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani,Jake Sullivan akipokelewa na Mkurugenzi wa masuala ya Amerika ya Kaskazini (katikati) Yang Tao wa wizara ya mambo ya nje ya ChinaPicha: Ng Han Guan/AFP/Getty Images

Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani,Jake Sullivan ameitembelea China, ni ziara yake ya kwanza nchini humo katika kipindi cha miaka minane. Sullivan amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Beijing na wawakilisho wa wizara ya mambo ya nje ya China pamoja na balozi wa Marekani mjini Beijing Nicholas Burns. Mshauri huyo wa masuala ya usalama wa rais Joe Biden amepangiwa kuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Ying katika ziara yake hiyo iliyopangwa kuendelea hadi Alhamisi.Xi: China na Marekani zapaswa kuwa washirika, sio washindani

China imesisitiza mara kadhaa juu ya umuhimu wa kufanyika mazungumzo kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu ambayo mahusiano yao yameharibika vibaya katika miaka ya hivi karibuni.China imesitisha mazungumzo ya kudhibiti silaha na Marekani

Miongoni mwa ajenda zinazotegemewa kujadiliwa ni migogoro ya Ukraine na Mashariki ya kati lakini pia mivutano iliyopo katika eneo la bahari ya Kusini mwa China na suala la Taiwan.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW