Msanii Sadat Nduhira nchini Uagnda ameanzisha mradi wa kuwafunza wasichana namna ya kutengeneza padi za kujistiri wakati wa hedhi kutokana na kwamba wasichana wengi nchini humo hawawezi kumudu gharama ya Padi za kawaida. Sadat anawasaidia kutengeneza padi hizo ili waweze kwenda shule wakiwa katika siku zao za hedhi bila wasiwasi wowote.