Shirika la Caritas kutoka Ujerumani linafadhili mradi wa kufundishia watoto wa jamii ya wafugaji na wakulima kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro nchini Tanzania. Walimu hutumia mazao ya shambani kama zana za kufundishia. Ifuatayo ni vidio fupi iliyopigwa na mwandishi wetu Dotto Bulendu.